Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » LEO KATIKA HISTORIA

LEO KATIKA HISTORIA

Written By Unknown on Saturday, 8 March 2014 | Saturday, March 08, 2014

Katika siku kama ya leo miaka 46 iliyopita, ilianza Harakati ya Ukombozi ya Moro dhidi ya utawala wa dikteta Ferdinand Marcos nchini Ufilipino. Dikteta Marcos alikuwa mshirika na muitifaki mkubwa wa Marekani na katika utawala wake wa kidikteta, maelfu ya Waislamu wa Ufilipino waliuawa au kufungwa jela. Baada ya Marcos kuondolewa madarakani mwaka 1986, harakati ya Moro ilikubali kutiliana saini makubaliano ya amani na serikali ya Manila. Hata  hivyo kulijitokeza matatizo katika utekelezwaji wa mkataba huo ambapo mwaka 1996 pande mbili zilitiliana saini makubaliano mapya. Kwa mujibu wa mkataba huo, Waislamu wa eneo la Waislamu la Mindanao walijipatia mamlaka ya kujitawala.
***
Miaka 29 iliyopita inayosadifiana na tarehe 8 Machi 1985, ulitokea mlipuko mkubwa wa bomu mjini Beirut, Lebanon na watu wasiopungua 45 waliuawa na wengine 175 kujeruhiwa. Mlipuko huo ulitokea karibu na msikiti unaotumiwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia.***
Siku kama ya leo miaka 43 iliyopita, wafanyakazi wa posta nchini Uingereza walirejea katika vituo vyao vya kazi baada ya kumaliza mgomo wao uliodumu kwa majuma saba. Wafanyakazi hao waligoma wakidai nyongeza ya mshahara ya asilimia 13. Mgomo huo katika Shirika la Posta nchini Uingereza ulilitia hasara shirika hilo ya Euro milioni 25.
***
Siku kama ya leo miaka 487 iliyopita alifariki dunia Ghiyathudeen Mansur mwanahisabati mashuhuri wa Kiirani. Ghiyathudeen Mansur alitumia sehemu kubwa ya umri wake kufundisha na kualifu vitabu.
***
Na miaka 1021 iliyopita kwa mujibu wa kalenda ya Hijria aliaga dunia mwanahisabati mashuhuri wa Kiislamu Abu Said Muhammad bin Abdul Jalil Sistani. Alimu huyo alikuwa amebobea katika nyuga za hisabati, jiometri na nujumu na alihesabiwa kuwa mwalimu mahiri wa taaluma hizo. Abdul Jalil Sistani aliiandikia kitabu  kuhusiana na kila elimu aliyojifunza na kuwapatia watu wengine ujuzi wake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi