Kocha wa Simba, Zdravok Logarusic, amesema kuwa mshambuliaji Hamis
Tambwe ni mahiri na hana mpinzani nchini Tanzania, hivyo anajivunia kuwa
ndani ya timu yake.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Logarusic alisema katika kikosi chake kinawachezaji wengi na washambulia lakini mshambuliaji huyo anatisha kutokana na ubora wake uwanjani.
“Ingawa nina wachezaji wengi wazuri ndani ya timu yangu, ila Tambwe ni kati ya vijana ninaojivunia kuwa nao, hivyo naamini yeye ni mmoja kati ya wale mahiri mno.
“Naamini mambo yatakuwa mazuri, japo kuwa kumekuwa na mapungufu kadhaa, ndio maana nimeamua kuweka programu mpya ya kuwaacha siku tatu katika ufanyaji wa mazoezi,” alisema.
Alisema, anaamini kwa nafasi hiyo aliyowapa wachezaji ya kutuliza
akili lakini wakiwa uwanjani itawasaidia katika mechi zinazofata,
akiamini kuwa mambo yatakuwa mazuri.
Simba inakabiliwa na mechi Machi 23 dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo ambao ulikuwa uchezwe Machi 12 lakini kutokana na mabadiliko ya kalenda ya mashindano yaliyofanywa na Shirikisho la Soka Nchini Tanzania (TFF) ili lazimika kusogezwa mbele.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Logarusic alisema katika kikosi chake kinawachezaji wengi na washambulia lakini mshambuliaji huyo anatisha kutokana na ubora wake uwanjani.
“Ingawa nina wachezaji wengi wazuri ndani ya timu yangu, ila Tambwe ni kati ya vijana ninaojivunia kuwa nao, hivyo naamini yeye ni mmoja kati ya wale mahiri mno.
“Naamini mambo yatakuwa mazuri, japo kuwa kumekuwa na mapungufu kadhaa, ndio maana nimeamua kuweka programu mpya ya kuwaacha siku tatu katika ufanyaji wa mazoezi,” alisema.
Simba inakabiliwa na mechi Machi 23 dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo ambao ulikuwa uchezwe Machi 12 lakini kutokana na mabadiliko ya kalenda ya mashindano yaliyofanywa na Shirikisho la Soka Nchini Tanzania (TFF) ili lazimika kusogezwa mbele.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!