Wizara ya Ulinzi ya Yemen imetangaza kuwa, wahajiri 42 wa Kiafrika
wanahofiwa kupoteza maisha, baada ya boti waliyopanda kuzama kusini mwa
pwani ya Yemen. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Yemen
imeeleza kuwa, boti iliyokuwa imebeba makumi ya wahajiri wa Kiafrika
ilizama karibu na pwani ya Biir Ali kusini mwa mkoa wa Shabwa. Taarifa
hiyo imeeleza kuwa, kikosi cha doria ya pwani kimefanikiwa kuwaokoa
wahajiri 30 na kuwapeleka kwenye kambi ya wakimbizi ya mji wa Mayfaa.
Taarifa zinasema kuwa, wahajiri kutoka Somalia na Ethiopia ambao
wanazikimbia nchi zao kutokana na kukithiri umasikini na mapigano,
wamekuwa wakipita Yemen na kuelekea Saudi Arabia. Takwimu zilizotolewa
na Shirika la Kimataifa la Wahajiri zinaeleza kuwa, karibu wahajiri elfu
themanini na nne kutoka eneo la Pembe ya Afrika wamekuwa wakipita
nchini Yemen na kuelekea katika nchi za Ghuba ya Uajemi na hasa Saudi
Arabia kwa shabaha ya kujitafutia kazi.
Home »
siasa kimataifa
» SOMA HII TAARIFA ILIYO TANGAZWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA YEMEN KUWA WATU WAPATAO 42 WENYE ASILIA YA AFRICA WAMEFARIKI DUNIA
SOMA HII TAARIFA ILIYO TANGAZWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA YEMEN KUWA WATU WAPATAO 42 WENYE ASILIA YA AFRICA WAMEFARIKI DUNIA
Written By Unknown on Monday, 10 March 2014 | Monday, March 10, 2014
Labels:
siasa kimataifa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!