Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM
vimefanikiwa kukomboa maeneo mengi ya kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Viongozi wa serikali ya Somalia wamesema kuwa, vikosi vya AMISOM
vikishirikiana na wanamgambo wanaofungamana na serikali ya Mogadishu
vimefanikiwa kukomboa sehemu kubwa ya eneo la Bakol lililoko kusini
magharibi mwa Somalia katika mpaka wa nchi hiyo na Ethiopia. Viongozi
hao wameeleza kuwa, hivi karibuni askari wa kulinda amani wa AMISOM
wakishirikiana na wanajeshi wa Ethiopia wamefanya operesheni ya pamoja
katika eneo la Rabdhure na kulikomboa eneo hilo kutoka mikononi mwa
wanamgambo wa kundi la al Shabab. Imeelezwa kuwa, kuanzia mwaka 2011
kundi la al Shabab lilipoteza udhibiti wake katika maeneo mengi ya
kusini na katikati mwa Somalia.
Home »
siasa afrika
» HATIMAYE MIKOA YA KUSINI MWA SOMALIA YASHIKILIWA NA VIKOSI VYA AMISOM
HATIMAYE MIKOA YA KUSINI MWA SOMALIA YASHIKILIWA NA VIKOSI VYA AMISOM
Written By Unknown on Monday, 10 March 2014 | Monday, March 10, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!