Serikali ya Afrika Kusini inafikiria uwezekano wa kuvunja kabisa
uhusiano wake wa kidiplomasia na Rwanda, baada ya serikali ya Kigali
kukumbwa na tuhuma za kufanya njama za kutaka kumuua mmoja wa makamanda
wa zamani wa jeshi la Rwanda nchini Afrika Kusini. Duru za kidiplomasia
kutoka Afrika Kusini zinaeleza kuwa, serikali ya Pretoria inaangalia
upya uhusiano wake wa kidiplomasia na Kigali na kuna uwezekano wa
kurudishwa nyumbani balozi wa Afrika Kusini aliyeko Kigali , na ubalozi
wa Rwanda kufungwa mjini Pretoria. Hivi karibuni, Afrika Kusini
iliwatimua wanadiplomasia watatu wa Rwanda wanaoshukiwa kupanga njama za
kumuuwa Jenerali Kayumba Nyamwasa, kamanda wa zamani wa Rwanda aliyeko
uhamishoni nchini Afrika Kusini. Rwanda nayo katika radiamali yake
iliamua kuwatimua wanadiplomasia sita wa Afrika Kusini walioko Kigali.
Imeelezwa kuwa, uhusiano wa pande mbili ulianza kuingia dosari tarehe 3
Machi mwaka huu, baada ya watu wenye silaha kuvamia nyumba ya Jenerali
Nyamwasa mjini Johannesburg na kupora mali kadhaa zikiwemo nyaraka na
kompyuta mpakato. Wakati wa uvamizi huo, Jenerali Nyamwasa hakuwemo
nyumbani. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi Disemba 2013 Kanali Patrick
Karegeya mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi ya Rwanda, aliuawa katika
mazingira ya kutatanisha nchini Afrika Kusini.
Home »
siasa afrika
» TAARIFA ZA CHINI CHINI ZASEMA KUWA UHUSIANO WA RWANDA NA AFRICA YA KUSINI WAWEZA KUVUNJIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA
TAARIFA ZA CHINI CHINI ZASEMA KUWA UHUSIANO WA RWANDA NA AFRICA YA KUSINI WAWEZA KUVUNJIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA
Written By Unknown on Monday, 10 March 2014 | Monday, March 10, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!