MSHAMBULIAJI wa
kimataifa wa Ujerumani, Lukas Podolski amesisitiza kuwa haogopi kuachwa
katika kikosi cha nchi hiyo kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia
lakini ana uhakika atachaguliwa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28
alipata majeruhi ya kuchanika msuli mwishoni mwa Agosti mwaka jana hatua
ambayo ilipelekea kumuweka nje mpaka mwishoni mwa jana huku akifanikiwa
kuanza katika mechi tano pekee katika klabu yake ya Arsenal msimu
huu. Wakati ikiwa imebaki miezi mitatu kabla ya kuanza michuano ya Kombe
la Dunia nchini Brazil, Podolski anajua anahitaji muda zaidi ili
kuonyesha kuwa anastahili nafasi katika kikosi hicho kinachonolewa na
Joachim Low lakini nyota huyo amesema ana uhakika na nafasi
yake. Akihojiwa kabla ta mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Chile baadae
leo Podolski amesema hana hofu juu ya nafasi yake katika kikosi cha
Ujerumani kwasababu ana uzoefu wa muda mrefu kwa kucheza mechi na
mashindano mengi. Podolski amesema baada ya kukaa nje kwa kipindi kirefu
hivi sasa yuko fiti na tayari ameshazungumza na makocha wote wawili wa
klabu na timu yake ya taifa. Ujerumani imepangwa kundi moja na timu za
Ureno, Ghana na Marekani katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa
kuanza kutimua vumbi Juni 12.
Home »
michezo ulaya
» SOMA KILE ALICHO KISEMA MWANASOKA PODOLSKI ANAE ICHEZEA ARSENAL KUHUSIANA NA TIMU YAKE YA TAIFA
SOMA KILE ALICHO KISEMA MWANASOKA PODOLSKI ANAE ICHEZEA ARSENAL KUHUSIANA NA TIMU YAKE YA TAIFA
Written By Unknown on Thursday, 6 March 2014 | Thursday, March 06, 2014
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!