Mazungumzo ya amani kati ya wawakilishi wa serikali ya Sudan
Kusini na waasi yamefanyika huko Addis Ababa Ethiopia lakini bila
kufikiwa natija yoyote. Mazungumzo hayo yalisimama tena jana huku pande
hizo hasimu zikishindwa kusaini makubaliano ya kimsingi, ambayo
yangetumika kama muongozo wa ajenda ya mazungumzo hayo.
Hussein Nyong msemaji wa upande wa waasi amesema, walikuwa tayari kusaini nyaraka ya mwongozo wa mazungumzo lakini upande wa serikali ukakataa na kuomba muda zaidi. Naye msemaji wa ujumbe wa serikali ya Juba Michael Makuei amesema kuwa, kwa bahati mbaya kujumuishwa kadhia ya washikiliwa 7 kama upande wa tatu katika mazungumzo hayo, kumesababisha kukwama duru hii ya mazungumzo. Itakumbukuwa kuwa, maelfu ya watu waliuawa na wengine karibu laki 9 kukimbia makazi yao kutokana na mapigano ya zaidi ya miezi miwili huko Sudan Kusini, kati ya vikosi vya serikali na waasi watiifu kwa Riek Machar makamu wa zamani wa rais.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!