Serikali ya Kenya inachunguza akaunti 20 za benki za ndani na za kigeni
ambazo polisi wanachukua kwamba zimetumika kufadhili shughuli za kigaidi
nchini humo, liliripoti gazeti la Daily Nation la Kenya siku ya
Jumatatu (tarehe 14 Aprili).
"Tunawachunguza baadhi ya wafuasi, taasisi za kifedha na wafadhili wakubwa wanaoshukiwa kufadhili harakati za kigaidi nchini," alisema Mkuu wa Polisi David Kimaiyo.
Akaunti hizo 20 zinazoshukiwa zilitambuliwa na kuwekewa alama kwa ajili ya upelelezi na Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID).
Mkurugenzi wa Idara hiyo, Ndegwa Muhoro, alisema akaunti hizo zilikuwa zikichunguzwa na Kitengo cha Uchunguzi wa Shughuli Haramu za Kibenki kwenye makao makuu ya CID jijini Nairobi. Alisema Kituo cha Ripoti za Kifedha, kilicho ndani ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, kimepokea taarifa juu ya shughuli zinazoshukiwa kuhusika na ugaidi, liliripoti gazeti la The Star la Kenya.
Wafanyabiashara kadhaa maarufu wa Mombasa ni miongoni mwa wale wanaochunguzwa kutokana na harakati hizo za kufadhili ugaidi.
"Kuna idadi kubwa ya kesi ambazo tunazifuatilia. Mara tu tukiwa na taarifa za uhakika bila shaka tutawapeleka mahakamani wale wanaohusika," alisema Muhoro, akiongeza kwamba wale watakaopatikana na hatia ya kufadhili ugaidi watashitakiwa kupitia Mkurugenzi wa Mashitaka.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!