Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » COACH WA BAYERN MUNICH PEP GUARDIOLA AWEKA WAZI KIWANGO CHA TIMU YAKE MBELE YA REAL-MADRID

COACH WA BAYERN MUNICH PEP GUARDIOLA AWEKA WAZI KIWANGO CHA TIMU YAKE MBELE YA REAL-MADRID

Written By Unknown on Wednesday, 16 April 2014 | Wednesday, April 16, 2014

Meneja wa klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola anaamini kuwa hawatakuwa na nafasi mbele ya Real Madrid katika mchezo wao wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kama hawatakuwa katika kiwango chao cha juu.
Bayern wamekuwa wakihangaika kurejea katika kiwango chao katika siku za karibuni ambapo wamefanikiwa kushinda mechi moja pekee kati ya tano walizocheza hivyo kumchanganya Guardiola. Akizungumza na vyombo vya habari Guardiola amesema kama wakicheza na Madrid kama walivyocheza katika mechi za karibuni hawatakuwa na nafasi ya kufika fainali. Kocha huyo ametoa hali ya tahadhari kuwa wako katika hali ya hatari na wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanarejea katika kiwango chao kabla ya kuivaa Madrid wiki ijayo. Mchezo wa mkondo wa kwanza baina ya timu hizo kwenye nusu fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu April 22 mwaka huu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi