Chama tawala cha African National Congress (ANC)
kilisisitiza wikendi kuwa Rais Jacob Zuma hakutumia pesa za Serikali
kujenga jumba lake la kibinafsi.
“Bado tunashikilia kuwa Rais hakuiba pesa zozote,” msemaji wa ANC Jackson Mthembu alisema.
Mthembu
alikuwa akizungumza baada ya ANC kuruhusiwa na Mahakama Kuu Johannesburg
kukata rufaa dhidi ya uamuzi kuhusu ujumbe mfupi uliotumwa na wakili wa
kiserikali kumshutumu Bw Zuma kwa kuiba pesa za umma wakati Serikali
ilipoimarisha usalama katika nyumba yake ya kibinafsi iliyo Nkandla,
mkoa wa Kwa Zulu-Natal.
Mnamo Machi
19, kiongozi wa mashtaka ya umma Thuli Mandondela alitoa ripoti ya
uchunguzi kuhusu madai ya ufujaji kuhusiana na nyumba ya Zuma.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!