Matatizo ya
matiti huwasumbua wanawake wengi na hata wanaume. Matatizo haya yapo ya
aina nyingi, mfano uvimbe wa matiti, maumivu ya matiti au matiti kutoa
maziwa au majimaji au damu. Tatizo hili hutokea katika umri wote kuanzia
pale mwanamke anapovunja ungo hadi anapofikia ukomo wa hedhi.
Matatizo ya matiti katika umri mkubwa kuanzia miaka 35 mara nyingi huambatana na saratani ya matiti. Jinsi tatizo linavyotokea Uvimbe wa matiti upo wa aina mbili. Kwanza ni vivimbe vidogo katika matiti na pili ni uvimbe mmoja mkubwa.
Vivimbe vidogo au mkubwa vinaweza kuwa katika titi moja au yote mawili. Uvimbe huu unaweza kuwa na maumivu au usiwe na maumivu na huwa unazunguka kama utaupapasa, endapo uvimbe utakuwa mgumu na hautembei kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa saratani.
Maumivu ya matiti hutokana na uvimbe kuwa mkubwa, kuvimba mishipa ya damu (Fibrocystic Breast Disease) na maambukizi ya matiti. Maambukizi na matatizo ya mishipa ya damu huwatokea zaidi wanawake wanaonyonyesha ambapo matiti huvimba na huwa na maumivu makali.
Tatizo la matiti kutoa maziwa au maji maji huwatokea zaidi wanawake ambao wamekatisha kunyonyesha, mfano mtoto amefariki au mimba imeharibika. Matiti yana maumbile tofauti kutokana na mtu na mtu, yanaweza kuwa makubwa au madogo, au makubwa wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua.
Dalili za matatizo Matatizo ya matiti huonyesha dalili tofauti tofauti kama tulivyoona hapo awali. Dalili hizi zinaweza kujitokeza kwa pamoja au mbili kwa pamoja au moja peke yake. Mfano mtu anaweza kuwa na maumivu na uvimbe au uvimbe na matiti kutoa maziwa.
Pia unaweza kuwa na dalili mojawapo ya hizo nilizoelezea, mfano maziwa kutoka pekee. Matatizo ya matiti huwa na uhusiano mkubwa na masuala ya uzazi, mfano mwanamke unaweza kuhisi matiti yanauma na yamejaa kipindi cha upevushaji mayai au unapokuwa mjamzito,
pia endapo matiti yatakuwa yanatoa maziwa na huna mimba wala historia ya ujauzito, basi ni matatizo ya mfumo wa homoni na uwezekano wa kushika mimba hupotea au haupo. Ni vema endapo una tatizo la matiti kutoa maziwa na unatafuta ujauzito hupati uwaone madaktari wa akina mama kwa uchunguzi wa kina.
Saratani ya matiti Tatizo hili huanza taratibu kama kivimbe kwenye titi moja au yote mawili. Uvimbe huu huendelea kukua taratibu na huwa sehemu moja ya titi. Katika hatua za awali, uvimbe hutembea yaani ukibonyeza unasogea sehemu nyingine na hauna maumivu.
Baada ya kuendelea kukua, uvimbe huwa mgumu kama ubao na hutanuka zaidi na kusababisha ngozi ya juu ya uvimbe huo kuwa na matundu au kama ganda la chungwa, tezi huvimba kwapani na wakati mwingine chuchu huanza kutoa damu.
Uchunguzi Matatizo ya matiti hufanyika katika vituo vya afya ambapo mgonjwa huchunguzwa kufuatana na jinsi tatizo linavyojitokeza. Vipimo vya damu, Ultrasound, X-ray na vingine vitafanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa.
Matibabu na ushauri Tiba hutegemea na jinsi vipimo vinavyoonyesha. Mgonjwa atatibiwa kadiri daktari atakavyomchunguza. Dawa za homoni na ufuatiliaji katika mfumo wa uzazi pia utafanyika. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!