Rio de Janeiro ni moja kati ya majiji ya Brazil ambayo baadhi ya
mechi za kombe la dunia zitafanyika mwaka huu huku maelfu ya wageni
wakijipanga kuingia jijini humo kupata burudani zote zitakazoambatana na
kile kilichowapeleka ‘FIFA World Cup 2014’.
Lakini kuna hatari kubwa katika jiji hilo hivi sasa ambapo kuna wizi uliokithiri unaofanywa na vibaka wa jiji hilo ambao wanaiba kwa mitindo na sehemu isiyodhaniwa. Wageni inabidi wawe makini kupitiliza ili vibaka wasiwageuze vibaka.
Mwanamke mmoja alikuwa akifanya mahojiano live na television ya RJTV katika mitaa ya Rio de Janeiro akitoa maoni yake kuhusu wizi uliokithiri katika eneo hilo alijikuta akikwapuliwa ghafla cheni yake ya dhahabu aliyokuwa ameivaa shingoni.
Hata hivyo, ripota aliyekuwa akimhoji alimtimua kibaka huyo ambaye aliitupa cheni hiyo na kutokomea huku akiwa ameiharibu kiasi fulani.
Tizama mwenyewe hapa kwenye hii video:

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!