Shirikisho la mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani,
limetangaza kumfungia maisha mmiliki wa klabu ya Los Angeles Clippers,
Donald Sterling kufuatia sakata la ubaguzi wa rangi ambalo liliibuka
mwishoni mwa juma lililopita.
Shirikisho la mpira wa kikapu nchini Marekani limefikia maamuzi hayo kufuatia uchungizi wa kina kubaini sauti iliyosikika kupitia mtandao wa TMZ ilikuwa ni ya mmiliki huyo ambayo amewachukiza watu mbalimbali wa michezo nchini humo akiwemo raisi Barack Obama.
Mbali na kufungiwa maisha kutojihusisha na mchezo wa mpira wa kikapu, pia shirikisho hilo limemtoza faini ya dola za kimarekani million 2.5 Donald Sterling, ikiwa ni sehemu ya adhabu ambayo inatumika kama fundisho kwa wabaguzi wengine dunaini kote.
Sterling, mwenye umri wa miaka 80, aliumbuka katika sakata la ubaguzi wa rangi, kufuatia sauti yake ambayo anasikika akimwambaia mwanamke mzungu kutojionyesha hadharani na wenzake wamarekani weusi.
Katika matamshi yanayosikika kwenye sauti ya Donald, yenye zaidi ya dakika nane imeendelea kujikita katika ubaguzi wa rangi ambapo alikua akimsisitiza mwanamke huyo mzungu aliyejipiga picha na marafiki zake wamarekani weusi wakihudhuria michezo ya Clippers.
Kwa kuonyesha ni vipi walivyochukizwa na kasumba hiyo ya ubaguzi wa rangi, wachezaji wa Los Angeles Clippers inayomilikiwa na Donald Sterling, walionekana wakiwa wamevaa jezi zao ndani nje ili kuficha nembo ya klabu hiyo wakati wakifanya mazoezi ya kujiandaa kwa mchezo wa hatua ya mtoano mwishoni mwa juma lililopita.
Tayari makampuni mbali mbali ya biashara, nayo yameshaondoa udhamini wao kwenye klabu hiyo, ikiwa ni ishara ya kuchukizwa na matamshi ya udhalimu wa ubaguzi wa rangi uliofanywa na Donald Sterling, anaeingia kwenye jela ya kutojihusisha na mchezo wa mpira wa kikapu katika maisha yake yote.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!