Nahodha
wa timu ya taifa ya Burundi ya Intamba kwenye mechi ya kirafiki kati ya
Burundi na Tanzania kwenye siku kuu ya sherehe za muungano, Didier
Kavumbangu amesaini Mkataba wa miaka miwili na
mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC mchana wa
mapema hapo jana,
Kavumbangu aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC, ameamua kusaini Azam FC baada ya kuona klabu yake haina mawasiliano naye licha ya kumaliza Mkataba wake.
Kavumbangu aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC, ameamua kusaini Azam FC baada ya kuona klabu yake haina mawasiliano naye licha ya kumaliza Mkataba wake.
Mchezaji wa kimataifa Didier Kavumbagu akisain mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Timu yake mpya ya Azam Fc ktk Msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara pamoja na mashimdano ya kimataifa |
“Mimi
ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini
viongozi hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,”
amesema Kavumbangu akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kusaini Mkataba
huo ambao unamfanya alipwe vizuri kuliko alivyokuwa analipwa Jangwani.
Pamoja
na hayo, Kavumbangu ameishukuru Yanga SC na mashabiki wayo kwa miaka miwili
aliyoichezea timu hiyo na anasema itabakia kwenye kumbukumbu zake kwa kuwa
ameshinda nayo mataji.
Mshambuliaji
huyo mrefu mwenye nguvu amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri
wake mpya, Azam FC ambako pia amepania kwenda kushinda mataji na
kuiwezesha timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na
familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.
“Mimi
sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida
yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba
moja wa Azam,”amesema.
Kavumbangu
alitua Yanga mwaka 2012 akitokea Atletico ya nchini Burundi na katika mechi
misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63
za mashindano yote, moja tu la penalti.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!