ALFAJIRI ya Alhamisi ya wiki iliyopita haitasahaulika nchini Tanzania kwa wakazi wa Jiji
la Dar es Salaam na viunga vyake ambapo maafa makubwa yalipoanza
kufuatia mafuriko ya mvua zilizonyesha mfululizo na kusababisha vifo na
uharibifu wa mali hivyo kuonesha wazi kuwa, kumbe Dar si salama.
Daraja linalounganisha wilaya ya Bagamoyo na Mkoa wa Dar es Salaam likiwa limekatika baada ya mvua hiyo kubwa kunyesha.Idadi ya vifo iliyoripotiwa mpaka juzi jioni ni kumi na mbili huku wanachi wengi wakikosa makazi na wengine kupotea kwa kusombwa na mafuriko.
Tukio la kwanza ni kuonekana laivu kwa maiti ya mtu mmoja aliyezolewa na maji maeneo ya Jangwani wilayani Ilala.Mbali na kushuhudia uharibifu wa kutisha wa miundombinu na mateso ya watu walioathirika.
Helkopta ya Jeshi la Wananchi iliyokuwa imebeba viongozi wa serikali ikiwa imeanguka baada ya kupoteza mwelekeo.
Baadhi ya barabara zikiwa zimefungwa kufuatia kujaa maji na madaraja kuvunjika na mengine kuzolewa. Barabara zilizofungwa ni pamoja na Dar es Salaam – Pwani kwa daraja la Mto Mpiji kubomoka.
Pia Barabara ya Dar- Kibiti ilifungwa na kufanya magari ya kwenda Kusini kutofanya safari kwa siku ya Jumapili iliyopita.
Daraja la Mto Ruvu lilifungwa kutokana na maji kupita juu ya daraja hivyo kufanya usafiri wa kutoka Dar kwenda mikoani kuwa mgumu sanjari na kuingia jijini Dar.
Ndani ya Jiji la Dar madaraja mengi yalijaa maji ikiwa ni pamoja la Kinyerezi, Mlalakua, Mpiji Magoe kwenda Kidimu, Mbezi Mwisho, Msewe Kimara, Kijichi na Jangwani.
Baadhi ya maeneo ya jiji hilo hasa Kigogo, Mwananyamala, Jangwani, Tandale,
Mabibo na Tabata yalikumbwa na kadhia ya maji kujaa kwenye makazi ya
watu na kusababisha wakazi wake kukaa kwenye mapaa kusubiri kuokolewa.
Makundi yaliyoonekana kupata wakati mgumu kwa mafuriko hayo ni wazee, wanawake na watoto waliokuwa wakishindwa kupanda juu ya mapaa ya nyumba, hivyo kusimama kwa kubebana kwenye maji kwa muda mrefu, waliopata bahati waliokolewa na watu wenye nguvu wakiwemo vijana.
Miili ilishuhudiwa ikipelekwa Hospitali ya Taifa Mubimbili kwa hifadhi huku ikiwa na dalili ya kuharibika.
Idadi kubwa ya majeruhi ambao hali zao zilikuwa mbaya walikimbizwa katika Hospitali za Amana, Mwananyamala na Temeke.
Maeneo mengi jijini Dar es salaam yameathirika, lakini ambayo hayako salama kabisa ni
mabondeni kama Jangwani, Kigogo Sambusa, Tabata ya Matumbi, Mikocheni
na Msasani.
Jumapili asubuhi, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik walipata ajali ya chopa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘JNIA’ walipokuwa wakijiandaa kwenda kutembelea sehemu zenye mafuriko.
Imebainika kuwa, miundombinu ya maji jijini Dar ndiyo sababu ya kutokea kwa mafuriko makubwa kwa vile maji hukosa njia ya kupita na kutengeneza visiwa vidogovidogo kila mahali.
“Kama mnavyoona Dar si salama, iko siku jiji lote litafunikwa na maji. Mvua kidogo mafuriko, watu wanakufa. Yaani vifovifo njenje,” alisema mkazi mmoja wa Mwananyamala Kisiwani baada ya kunusurika na mafuriko.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!