Miaka 18 iliyopita katika siku kama ya leo yaani tarehe 18 Aprili
1996, jeshi la anga la utawala wa Kizayuni wa Israel lilishambulia kituo
cha kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika kijiji cha
Qana, kusini mwa Lebanon. Katika shambulizi hilo la kinyama la Wazayuni,
zaidi ya raia 100 wa Lebanon waliuawa shahidi wakiwemo wanawake na
watoto.
******************************************************************
Siku kama ya leo miaka 34 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 18 Aprili 1980, Zimbabwe ambayo wakati ule ilikuwa ikijulikana kwa jina la Rhodesia, ilipata uhuru. Zimbabwe ilikoloniwa na Uingereza mwishoni mwa karne ya 19. Mara baada ya Vita vya Pili vya Dunia na kufuatia kudhoofika Uingereza, zilianza harakati za wananchi za kupigania uhuru na hatimaye harakati hizo zilipelekea kuundwa makundi ya mapambano ya silaha. Zimbabwe ina ukubwa wa kilomita mraba 390,000 na inapakana na nchi za Msumbiji, Zambia, Botswana na Afrika Kusini.
*****************************************************************
Na miaka 59 iliyopita katika siku kama hii ya leo ulifanyika mkutano wa kwanza wa wawakilishi wa nchi za Asia na Afrika katika mji wa Bandung nchini Indonesia. Mkutano huo uliowashirikisha wajumbe kutoka zaidi ya nchi 29 za Asia na Afrika, ulikuwa na lengo la kujenga umoja wa nchi hizo za ulimwengu wa tatu katika kukabiliana na kambi kubwa mbili duniani za Mashariki na Magharibi. Mkutano huo wa Bandung ndio ulioandaa mazingira ya kuundwa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM).

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!