Wananchi wa Tunisia wamefanya maandamano dhidi ya utawala haramu wa
Kizayuni na kuichoma moto bendera ya utawala huo. Maandamano hayo
yalifanyika jana mjini Tunis huku washiriki wa maandamano hayo
wakitangaza kushikamana na wananchi madhlumu wa Palestina. Watunisia
walitaka pia kuachiliwa huru maelfu ya wafungwa wa Kipalestina ambao
wanaendelea kushikiliwa katika korokoro za kutisha za utawala huo
pandikizi.
Aidha waandamanaji hao wamechoma moto bendera ya utawala huo wa Kizayuni na kutangaza kuwaunga mkono wananchi wa Palestina. Walilaani ukandamizaji wa kuchupa mipaka wa askari wa utawala wa Kizayuni dhidi ya wafungwa wa Kipalestina na kutaka kuachiliwa huru wafungwa hao. Aidha waandamanaji waliunga mkono mugawama wa wananchi madhlumu wa Palestina mbele ya utawala wa Kizayuni. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu 150 walio chini ya umri wa kisheria wa miaka 18 wanashikiliwa katika jela za kuogofya za Israel bila ya kufunguliwa mashitaka.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!