KUUMIA KWA KIPA PETER CZECH NI PIGO KUBWA KWA CHELSEA
Mlinda mlango wa Chelsea,Petr Cech atakosa
sehemu yote ya msimu iliyobakia mara baada ya kupata jeraha la bega
katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Ulaya
waliyotoka sare ya 0-0 dhidi ya Atletico Madrid.
Nahodha,John Terry hawezi kucheza tena kabla ya fainali ya Lisbon
kama Chelsea watafanikiwa kufika hatua hiyo mara baada ya kupata
majeraha kwenye dimba la Vicente Calderon katika kipindi cha pili.
Jose Mourinho alithibitisha baada ya mchezo kuwa Cech ambaye
alilazimika kutolewa katika dakika ya 18 hawezi kurudi uwanjani tena kwa
kipindi chote kilichosalia cha kampeni.
Safu ya ulinzi ilimgharimu Mourinho baada ya Cech kupata jeraha
kipindi cha kwanza na Terry baadae kutolewa baada ya dakika 72 kutokana
na matatizo ya mguu.
Pia viungo Frank Lampard na John Obi Mikel walipewa kadi za njano
hivyo kufanya kufungiwa kutocheza mchezo wa marudiano utakaopigwa
Jumatano ijayo.
Cech alipata jeraha wakati akijaribu kuokoa mpira chini ya mwamba wa
juu wa goli lake ambapo David Luiz alimsukuma Raul Garcia ambaye
alimgonga mlinda mlango huyo na kumfanya adondoke chini vibaya hivyo
kumsababishia maumivu ya bega yaliyomlazimu atolewe na nafasi yake
kuchukuliwa na Mark Schwarzer.
Raia huyo wa Jamhuri ya Czech sasa atakosa michezo mitatu iliyosalia
ya ligi kuu ya Uingereza akianzia mchezo dhidi ya vinara wa ligi
hiyo,Liverpool Jumapili pamoja na mchezo wa marudiano dhidi ya kikosi
cha Diego Simeone utakaopigwa Stamford Bridge na wa fainali ya Mei 24
endapo watafanikiwa kuingia.
Mourinho alisema”Msimu wa Petr Cech umekwisha.Usiniulize kitaalamu lakini msimu umeisha kwake.”
Mreno huyo akaongeza kuwa,”Tunapaswa kuingia fainali ili John aweze kucheza na sisi.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!