Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema kuwa ni mapema sana kusema iwapo
atagombea urais kwa kipindi cha tatu na kwamba muda utakapowadia
atawaeleza wananchi.
Kagame amesema hayo akijibu swali la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tufts karibu na Boston, Marekani. Rais wa Rwanda amesema kuwa, amekuwa akiulizwa ni lini ataondoka madarakani tangu aliposhika wadhifa huo na kwamba yupo kwa ajili ya kuwawakilisha Wanyarwanda.
Katika hotuba yake hiyo ambayo lengo lake lilikuwa ni kueleza jinsi Rwanda inavyojikwamua na athari za mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, Kagame amesema kuwa, wamejifunza kwamba watu wanapaswa kukubali mambo waliyoyatenda na kwamba iwapo watategemea wageni basi wataangamia. Kagame pia ameituhumu jamii ya kimataifa kwa kuchangia kukosekana amani na usalama katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuruhusu watu waliofanya mauaji ya kimbari nchini Rwanda kukimbilia katika milima ya mashariki mwa Kongo na kuwapatia silaha.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!