Siku kama ya leo miaka 450
iliyopita alizaliwa William Shakespeare, mshairi na mwandishi mashuhuri
wa michezo ya kuigiza wa Uingereza. Shakespeare alianza kazi zake za
usanii sambamba na kushiriki katika michezo ya kuigiza. Alipata
umashuhuri mkubwa katika fani hiyo. Kazi zake za kisanii zilikuwa
mchanganyiko wa sanaa iliyoakisi majonzi na vichekesho.
Miongoni mwa kazi maarufu za
Shakespeare ambazo zinaorodheshwa kati ya kazi bora zaidi za waandishi
wa drama duniani ni Hamlet, King Lear na Romeo na Juliet.
*****************************************************************
Tarehe 23 Aprili miaka 156
iliyopita alizaliwa mwanafizikia Max Plank wa Ujerumani ambaye pia
alikuwa mtaalamu wa hesabati aliyebuni nadharia ya kwanta katika elimu
ya fizikia. Mwaka 1918 Max Plank alitunukiwa tuzo ya fizikia ya Nobel
kwa kugundua nadharia ya kwanta. Plank ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa
dikteta wa zamani wa Ujerumani Adolph Hitler, alifanya utafiti mkubwa
katika nyanja za mwendojoto (sayansi ya uhusiano wa joto na kazi za
mitambo) fizikia nadharia, joto, mnururisho na nuru na kuandika vitabu
kadhaa katika medani hiyo.
*****************************************************************
Na siku kama ya leo miaka 22
iliyopita, inayosadifiana na tarehe 23 Aprili 1992, alifariki dunia
Satyajit Ray mwandishi na mtengeneza filamu mashuhuri wa India. Satyajit
Ray alizaliwa mwaka 1921, na filamu zake za kijamii ziligusa zaidi
hisia za jamii ya wananchi wa nchi hiyo, na kupelekea kupendwa zaidi na
wananchi wa India.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!