Mkutano wa kimataifa wa kudhibiti intaneti unatarajiwa
kuanza leo nchini Brazil baada ya kufichuliwa udukuzi unavyofanywa na
Marekani dhidi ya nchi nyinginezo.
Wawakilishi kutoka nchi mbalimbali duniani watakaoshiriki
mkutano huo wa siku mbili mjini Sao Paulo, wanatarajiwa kuweka sheria za
kudhibiti intaneti huku baadhi ya nchi zikipanga kuunda chombo cha
kimataifa kitakachodhibiti kazi za kiufundi mitandaoni.
Hivi sasa Marekani ndio inayosimamia Mtandao wa Dunia
Nzima (World Wide Web) lakini nchi nyingi zinahisi kughilibiwa baada ya
kufichuliwa vitendo vya kijasusi vinavyofanywa na mashirika ya kijasusi
ya Marekani mitandaoni.
Hayo yamejiri ikiwa ni miezi mitatu tangu Edward Snowden,
wafanyakazi wa zamani wa Shirika la Usalama la Marekani (NSA) aanike
hadharani kwamba mashirika mawili ya kijasusi ya nchi hiyo yanasikiliza
mazungumzo ya simu na mitandanoni ya mamiliaoni ya watu barani Ulaya na
kwingineo duniani.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!