Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SHIRIKA LA AMNESTY LAIKOSOWA QATAR

SHIRIKA LA AMNESTY LAIKOSOWA QATAR

Written By Unknown on Wednesday, 23 April 2014 | Wednesday, April 23, 2014

Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limeokosoa serikali ya Qatar kwa kushindwa kuwalinda wafanyakazi wa kigeni wanaofanya kazi za ndani kutokana na unyonyaji mkubwa wanaofanyiwa nchini humo.
Taasisi hiyo ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu imesema kuwa, wafanyakazi wahajiri katika nchi hiyo ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi wanateswa, kulazimishwa kufanya kazi, kuchoshwa kwa kazi za muda mrefu na kunyanyaswa kwa maneno, kimwili na kijinsia. Ripoti iliyotolewa na  Amnesty International  imeeleza kuwa baadhi ya wanawake wanashurutishwa kufanya kazi hadi masaa 100 kwa wiki bila ya kupewa siku ya kupumzika huku wengine wakizuiwa kutoka nje ya nyumba kwa ujumla. Pia imeelezwa kwamba, wafanyakazi wa kigeni nchini Qatar wanakabiliwa na sheria za kibaguzi zinazowanyima haki muhimu za kuwalinda na hivyo kunyonywa na kunyanyaswa kutokana na kazi za kulazimishwa na biashara haramu ya watu. 
Wanawake 84,000 wamepelekwa nchini Qatar kufanya kazi za ndani, wengi wao kutoka nchi za Kusini na Kusini mashariki mwa bara la Asia.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi