MAGAIDI WA SYRIA WAPEWA SILAHA KUBWAKUBWA NA UTURUKI
Shirika la kijasusi la Uturuki (MIT) limewapatia makombora dhidi ya
vifaru wapiganaji wanaoendesha mapigano dhidi ya serikali ya Rais Bashar
al Assad wa Syria. Uturuki imetoa makombora hayo dhidi ya vifaru
yaliyotengenezwa nchini Marekani kwa magaidi hao wa Syria wanaoungwa
mkono na nchi za kigeni. Gazeti la Aydinlik linalochapishwa nchini
Uturuki limeeleza kwenye ripoti yake kuwa, Salim Idris kamanda wa jeshi
linalojulikana kwa jina la Free Syrian Army (FSA) ndiye aliyekuwa na
nafasi kuu katika kufanikisha upelekaji wa makombora hayo kutoka Uturuki
na kuwafikia magaidi huko Syria.
|
Salim Idris |
Ripoti ya gazeti la Aydinlik imeongeza
kuwa, magaidi wasiopungua 12 wamepewa mafunzo huko Uturuki ya jinsi ya
kutumia silaha hizo. Uamuzi huo wa kuyahamisha makombora hayo dhidi ya
vifaru kutoka Uturuki hadi nchini Syria ulichukuliwa baada ya kufanyika
mazungumzo mwaka jana kati ya Idris kamanda wa Free Syrian Army (FSA) na
Seneta wa chama cha Republican John McCain.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!