Hatu ya wakuu wa utawala haramu wa Israel ya kukaidi matakwa ya
kimatiafa kuhusu kuheshimu misingi ya awali kabisa ya haki za binaadamu
ni jambo ambalo sasa limepelekea hata muitifaki wa karibu kabisa wa Tel
Aviv, yaani Marekani kuingiwa na wasi wasi kuwa Israel itabadilika na
kuwa utawala wa ubaguzi wa rangi au Apartheid. John Kerry Waziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani hivi karibuni amesema kuwa iwapo Israel
haitakubali pendekezo la kuundwa nchi mbili huru katika ardhi za
Palestina zinazokaliwa kwa mabavu basi katika siku za usoni utawala wa
Tel Aviv utageuka na kuwa utawala wa ubaguzi wa rangi. Huu unahesabiwa
kuwa ukosoaji mkali zaidi hadi sasa wa wakuu wa Marekani kwa muitifaki
wao, Israel. Pamoja na matamshi hayo ya Kerry kile kilicho wazi ni kuwa
tokea kuundwa utawala haramu wa Israel, utambulisho wake umekuwa ni wa
ubaguzi wa rangi sawa na ule wa makaburu waliotimuliwa Afrika Kusini.
Wazayuni wana mtazamo potofu kuhusu dini ya Uyahudi na Kitabu cha
Taurati. Wanaamini kuwa kaumu ya Mayahudi ni bora kuliko kaumu na dini
zingine zote duniani. Kwa hivyo tunaweza kusema kuwa hata kabla ya
kuundwa utawala bandia wa Israel mwaka 1948, Uzayuni ulikuwa sawa na
ubaguzi wa rangi na kikaumu. Historia ya kukaliwa kwa mabavu Palestina
na kuundwa makundi ya Mayahudi wahajiri ni jambo lililoanza mwanzoni mwa
karne ya 20. Katika kipindi hicho Wazayuni walikuwa na nadharia
iliyokita mizizi kuhusu kutenganishwa watu kwa msingi wa rangi. Mwanzoni
mwa karne ya 20 Wazayuni walifanya juhudi za kuunda jamii mbili
tafauti. Moja ilikuwa ni ya Wapalestina Waarabu waliowengi ambao
aghalabu ni masikini na walioishi katika hali ngumu na katika upande wa
pili ni jamii ya Mayahudi wahajiri wenye utajiri mkubwa pamoja na kila
kitu walichohitajia mbali na kushikilia hatamu za utawala. Leo baada ya
kupita miaka 70 tokea Mayahudi waikalie kwa mabavu ardhi ya Palestina,
tunashuhudia zaidi ya wakati wowote ule kudhihiri kwa kiwango kikubwa
ubaguzi wa rangi Israel. Ujenzi wa ukuta wa kibaguzi katika Ukingo wa
Magharibi wa Mto Jordan ni mfano wa wazi kabisa wa sera za kibaguzi za
kuwatenganisha Wapalestina na Mayahudi. Aidha ujenzi wa vitongoji vya
Walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu
mwaka 1967, mbali na kuwa kinyume cha sheria za kimataifa pia
kunafanyika kwa lengo la kuwatenganisha kibaguzi wakaazi wa eneo hilo.
Ujanja waliotumia wakuu wa Israel katika kufunika utawala wao wa
kibaguzi ni kuruhusu Waarabu waishio katika ardhi zao zilizoporwa mwaka
1948 kuwa na wajumbe katika Bunge la Israel, Knesset. Pamoja na hayo,
wale wote wanaokuja madarakani Israel huwa na ndoto ya muda mrefu ya
kuwatimua kikamilifu Waarabu na Waislamu kutoka Israel na kuunda dola
wanaloliita la Kiyahudi. Wakuu wa Israel hutamka lengo lao hilo la
kibaguzi pasina kuwa na wasi wasi. Iwapo maneno kama hayo yangetamkwa
sehemu nyingine duniani yangehesabiwa kuwa ni jinai ya kujitangazia
ubora wa kikaumu na kidini. Lakini huko Israel kuwasilishwa pendekezo la
kuwafukuza Waarabu na Waislamu katika ardhi zao za jadi si tu kuwa
hakulaaniwi bali wanaotoa pendekezo hilo la ubaguzi wa rangi na kidini
hutunukiwa zawadi na kupewa cheo cha waziri wa mambo ya nje. Kwa maelezo
hayo sera za kibaguzi za Israel ziko wazi na haziwezi kufichika. Hii
ndio sababu hata Umoja wa Mataifa pamoja na kuwa unadhibitiwa na
waitifaki wa Israel yaani Marekani na nchi za Ulaya, ulitangaza kuwa
Uzayuni ni sawa na ubaguzi wa rangi. Hivi sasa mkuu wa chombo cha
diplomasia cha serikali ya sasa ya Marekani ambayo inahesabiwa kuwa
serikali tiifu zaidi kwa Israel, imeonya kuwa ukaidi wa Tel Aiv unaweza
kuibadilisha Israel kuwa utawala wa kibaguzi. Suala hili linaaonyesha ni
kiasi gani Israel ilivyotengwa duniani hata na muitifaki wake wa karibu
zaidi.
Home »
siasa kimataifa
» MAREKANI YAPATWA NA HOFU KUHUSU TABIA YA UBAGUZI YA ISRAEL
MAREKANI YAPATWA NA HOFU KUHUSU TABIA YA UBAGUZI YA ISRAEL
Written By Unknown on Monday, 28 April 2014 | Monday, April 28, 2014
Labels:
siasa kimataifa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!