Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » LEO KATIKA HISTORIA

LEO KATIKA HISTORIA

Written By Unknown on Monday, 28 April 2014 | Monday, April 28, 2014

miaka 22 iliyopita katika siku kama ya leo, makundi ya mujahidina wa Afghanistan hatimaye yalipata ushindi baada ya kuendesha mapambano ya miaka 13 baina yao na jeshi la Urusi ya zamani na serikali ya kibaraka ya nchi hiyo. Baada ya majeshi ya Urusi ya zamani kuikalia kwa mabavu nchi hiyo kwa miaka 13, hatimaye mwezi Februari mwaka 1989 wanajeshi hao wa Urusi walilazimika kuondoka Afghanistan. Hata hivyo kutokana na makundi hayo ya Kiafghani kutokuwa na mikakati mizuri na pia kutopata misaada kutoka nje, vikosi vya serikali ya Afghanistan viliendelea kubakia madarakani chini ya uungaji mkono wa kifedha na kijeshi wa Urusi ya zamani.

 ****************************************************************

Siku kama ya leo miaka 459 iliyopita, Kongamano la Augsburg lilifanyika katika mji wenye jina hilo huko nchini Ujerumani. Katika kongamano hilo, viongozi wa Kikatoliki chini ya uongozi wa Papa Paul IV (wa Nne) kwa mara ya kwanza waliunga mkono uhuru wa madhehebu ya Waprotestanti. Aidha katika kongamano hilo ulichukuliwa uamuzi wa kurejeshwa mali za Waprotestanti walizokuwa wamenyang'anywa. Hata hivyo uamuzi huo haukutekelezwa na hivyo kuzusha vita vya miaka kumi kati ya Waprotestanti na Wakatoliki katika nchi mbalimbali za Ulaya.

 ****************************************************************

Na miaka 49 iliyopita katika siku kama ya leo, Marekani kwa kutumia kisingizio cha kuwalinda raia wake, iliishambulia kijeshi nchi ya Dominican. Kabla ya mashambulizi hayo wananchi wa Dominican walikuwa wameanzisha mapambano dhidi ya watawala wa kidikteta waliokuwa wakitawala katika nchi hiyo. Kutokana na kundi la wanajeshi kuungana na wanamapinduzi hao, hatimaye jeshi na utawala wa kidikteta wa nchi hiyo lilishindwa vibaya katika mapambano hayo. Awali Marekani ilipeleka wanajeshi 1500 nchini Dominican kwa lengo la kupambana na wananchi wa taifa hilo na katika kipindi kifupi tu vikosi hivyo vikaongezeka na kufikia elfu 40. Huku ikisadiwa na manowari za kijeshi hatimaye Marekani ilifanikiwa kuizingira nchi hiyo. Hata hivyo baada ya wanamapinduzi wa nchi hiyo kuunda serikali Marekani ililazimika kuondoka nchini Dominican.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi