Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » UMOJA WA MATAIFA WAOMBA PANDE MBILI ZINAZO PIGANA NCHINI SUDAN KUSINI KUSIMAMISHA MAPIGANO

UMOJA WA MATAIFA WAOMBA PANDE MBILI ZINAZO PIGANA NCHINI SUDAN KUSINI KUSIMAMISHA MAPIGANO

Written By Unknown on Friday, 25 April 2014 | Friday, April 25, 2014

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka pande zinazopigana Sudan Kusini kusitisha mapigano hayo.
Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alkhamisi ya jana walitoa taarifa ambayo imeeleza wasiwasi wa baraza hilo kuhusu machafuko ya ndani huko Sudan Kusini na kutishia kuziwekea vikwazo pande mbili hasimu nchini humo iwapo hazitasitisha mienendo isiyo ya kibinadamu.
Taarifa ya Baraza la Usalama imesisitiza kuwa serikali ya Rais Salva Kiir huko Sudan Kusini inawajibika kulinda maisha ya raia wa nchi hiyo. Taarifa hiyo pia imewataka wapinzani wa serikali ya Juba kusitisha mauaji ya raia la sivyo watakabilia na hatua kali za Baraza la Usalama la Umoja Mataifa.
Mkuu wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous amesema kuwa pande hasimu nchini Sudan Kusini zinapaswa kuheshimu mada za makubaliano ya kusitisha machafuko yaliyotiwa saini na pande hizo mbili.
Sudan Kusini ilitumbukia katika vita na machafuko ya ndani Disemba 15 mwaka jana baada ya Salva Kiir kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar kuwa alifanya jaribio la kupindua serikali yake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi