PENZI la lina nguvu sana usisikie. Kwa binti wa Kialgeria,
mrembo Wahiba, Franck Ribery hakuwa na ujanja na hatimaye alikubali
kubadili dini na kuwa Mwislamu.
Mrembo huyo ndiye alichochea Ribery kubadili dini na jina lake la Kiislamu anaitwa Bilal Yusuf Mohammad.
Hayo ni maisha yake. Kwenye soka, mahali ambapo
wengi wanamfahamu Ribery, staa huyo ni hatari. Mkongwe wa soka nchini
Ufaransa ambaye kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa Real Madrid, Zinedine
Zidane, aliwahi kumtaja Ribery kuwa ni dhahabu ya soka la Ufaransa.
Soka ndicho kitu kilichomfanya Ribery kuwa maarufu
na umahiri wake wa uwanjani umemfanya kuwa mmoja ya wanasoka wanaolipwa
vizuri duniani.
Winga huyo wa Bayern Munich na timu ya taifa ya
Ufaransa, aliyezaliwa Aprili 7, 1983, anatajwa kuwa na kipato
kinachokadiriwa kuwa Dola 40 milioni.
Jinsi alivyopiga pesa
Chanzo kikubwa cha kipato cha Ribery kinatokana na
soka. Ribery anavuna mshahara wa nguvu klabuni Bayern Munich. Mwaka
jana, staa huyo aliripotiwa kupanda mshahara kwa Euro 7 milioni kwa
mwaka kutoka Euro 3.75 milioni.
Hilo lilikuwa ongezeko kubwa la mshahara ambapo
kabla ya kodi alidaiwa kupokea Euro 10 milioni. Taarifa nyingine
zilibainisha kuwa mshahara wa Ribery ulikuwa Pauni 8.5 milioni kwa mwaka
sawa na Pauni 164,000 kwa wiki.
Hata hivyo, vyovyote itakavyokuwa bado kiwango hicho cha pesa anazopokea staa huyo ni kikubwa.
Ukiweka kando kupiga pesa kwa kupitia mishahara,
Ribery pia amekuwa na dili nyingine za mikataba ya udhamini ambayo
imekuwa ikimpa manufaa makubwa pia. Baadhi ya kampuni zinazomdhamini
staa huyo ni Nike na EA Sports.
Ribery pia anapiga pesa kupitia kipindi chake cha
televisheni nchini Ufaransa kinachofahamika kwa jina la ‘The Franck
Ribery Show’ ambacho kimekuwa kikivutia wadhamini wengi.
Kipindi hicho cha televisheni kinaonyeshwa kupitia kituo cha Direct 8 na kilikuwa kikidhaminiwa na Nike.
Mei 2010, bango lenye picha ya Ribery lenye ukubwa
wa futi 89 kwa 98 liliwekwa kwenye mji wa Boulogne-sur-Mer alikozaliwa
staa huyo na alikuwa akilipwa pesa. Hiyo ilikuwa kabla ya fainali za
Kombe la Dunia za mwaka 2010.
Maisha binafsi na ndoa
Maisha binafsi na ndoa
Ribery, utotoni mwake alikumbana na matatizo
mengi. Akiwa na umri wa miaka miwili tu, yeye na familia yake walipata
ajali katika mji wa nyumbani kwao baada ya magari kugongana. Ribery
alitokea dirishani na kwenda kuangukia uso ambapo alipata jeraha kubwa
usoni.
Pamoja na kupata pesa ambazo angeweza kufanya
upasuaji na kuondoa kovu lililopo usoni mwake, lakini Ribery ametaka
kovu hilo libaki kama lilivyo kwa sababu mwenyewe anaamini linampa nguvu
na hasira ya kupambana na maisha.
Ribery ambaye anavaa kiatu namba 42, ameoana na
mrembo mwenye asili ya Algeria na kufanikiwa kuzaa naye watoto watatu,
wa kike wawili; Hizya alizaliwa 2005, Shaninez alizaliwa Januari 2008 na
wa kiume Seif, aliyezaliwa Septemba 2011.
Ribery aliwahi kukumbwa na kashfa ya ngono baada
ya kudaiwa kufanya ngono na binti mwenye umri mdogo, Zahia Dehar, ambaye
alikuwa akijihusisha na ukahaba.
Kutokana na kuvuna pesa nyingi, Ribery na familia
yake wamekuwa wakiishi kwenye majumba yenye hadhi kubwa na kutembelea
magari ya kifahari akifurahia matunda ya kazi yake nzuri uwanjani.
Ribery amekuwa akifahamika kwa majina ya utani ya ‘The Magician’, ‘Ferraribery’, ‘Scarface’ na ‘Flagada’.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!