Nahodha wa Liverpool,Steven Gerrard alisema
kuwa ushindi mzuri dhidi ya Manchester City ni salamu kama timu katika
kujiandaa kuwakumbuka waathirika wote wa Hillsborough pamoja na familia
zao.
Kiungo huyo naye alikuwa akimkumbuka binamu
yake,Jon-Paul Gilhooley aliyekuwa na umri wa miaka 10 ambaye ndiye
alikuwa kijana mdogo zaidi kati ya watu 96 waliopoteza maisha yao katika
janga lililotokea uwanjani pale Sheffield.
Gerrard aliweza kumwaga machozi mara baada ya
ushindi wa goli 3-2 Jumapili ambao uliweza kuipa matumaini makubwa
Liverpool kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza.
Jana ililikuwa ni miaka 25 ya kuwaenzi mahanga hao na Gerrard alikuwa katika sehemu ya kuwakumbuka waathirika hao pale Anfield.
Huku akisema,”Sababu iliyonipa mguso mkubwa ilikuwa kwasababu jinsi mchezo dhidi ya Man City ulivyokuwa na hisia.”
“Haikuwa tu sababu ulikuwa mchezo mkubwa katika msimu wetu,ilikuwa
sababu wiki hii mara zote ni kuhusu kitu zaidi soka kwa kila mmoja
ambaye anahusika na Liverpool.Ni mguso mkubwa kwa watu wengi.”Gerrard akaongeza kuwa,”Naongea kwa uhuru wa kila mmoja pale naposema ushindi ulikuwa salamu kwa waathirika wa Hillsborough pamoja na familia zao.”
“Kila mchezaji atakuwepo katika maadhimisho hayo kuonyesha na kulipa heshima kama tunavyotakiwa kuwa.”
Brendan Rogders alikuwepo katika hafla hiyo na alipewa nafasi ya kusoma lisala ndefu mbele ya halaiki ya watu wote walioudhuria.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!