Kocha wa timu ya taifa
ya Ufaransa, Didier Deschamps haamini kuwa timu kama timu yake inapewa
nafasi ya kunyakuwa Kombe la Dunia linatarajiwa kuanza kutimua vumbi
Juni mwaka huu. Ufaransa iling’olewa katika hatua ya makundi katika
michuano hiyo mwaka 2010 huku wakifuzu kwenda Brazil baada ya kuifunga
Ukraine katika mechi ya mtoano na Deschamps anafikiri timu hiyo sio
tishio tena kama zilivyo timu zingine hivi sasa. Deschamps amesema kuna
timu sita au saba ambazo zinakwenda katika michuano hiyo kushinda lakini
Ufaransa haiku katika orodha hiyo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa
madhumun yao ni kushinda mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Honduras
utakaochezwa Juni 15 na baadae kuendelea kushinda kufanya hivyo kwa kila
mchezo utakaofuata.
Home »
michezo ulaya
» UFARANSA HAINA UWEZO WAKUNYAKUWA KOMBE LA DUNIA:DESCHAMPS
UFARANSA HAINA UWEZO WAKUNYAKUWA KOMBE LA DUNIA:DESCHAMPS
Written By Unknown on Wednesday, 16 April 2014 | Wednesday, April 16, 2014
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!