Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » SHERIA YA KUUZA KIFAA CHAKUPIMA UKIMWI MAJUMBANI YAPITISHWA NCHINI UINGEREZAA

SHERIA YA KUUZA KIFAA CHAKUPIMA UKIMWI MAJUMBANI YAPITISHWA NCHINI UINGEREZAA

Written By Unknown on Monday, 7 April 2014 | Monday, April 07, 2014

Serikali ya Uingereza imepitisha sheria inayoruhusu uuzaji wa kifaa  cha kupimia virusi vya ukimwi kwa watu binafsi ili kuwawezesha kujifanyia vipimo vya ukimwi wawapo majumbani kwao.
Serikali hiyo ilikuwa imeruhusu ufanyaji wa vipimo vya ukimwi majumbani tangu September mwaka jana lakini sheria rasmi imeanza kufanya kazi Jumapili hii.
Hata hivyo, vifaa hivyo ambavyo vitakuwa vinafanya kazi kwa kuchukua tone dogo la damu kwenye kidole cha mhusika havipo Uingereza kwa sasa, lakini kituo cha Terrence Higgins Trust HIV Charity kimesema kuwa majaribio ya kifaa hicho yanaweza kuanza nchini humo mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka 2015.
Imeripotiwa kuwa kuwepo kwa kipimo hicho kutasaidia idadi inayokadiriwa kuwa wananchi zaidi ya 25,000 wanaoishi na VVU lakini bado hawajapimwa na wataweza kufahamu afya zao kirahisi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi