Mwimbaji wa Hips Don’t Lie, Shakira ameamua kuiweka sawa kauli yake
kuhusu kile kilichotafsiriwa kuwa ni wivu mkubwa alionao mpenzi wake
Gerard Pique kwa kumkataza kufanya video na wanaume wenye mvuto.
Shakira aliteka vichwa vya habari baada ya kumaliza mahojiano na Billboard ambapo alieleza kuwa mpenzi wake huyo ambaye ni mwanasoka amemuwekea mipaka ya kutosha na kwamba kwa kuwa alimkataza kufanya videos na wanaume ame amua kufanya na wanawake.
Hii ilitafsirwa na wengi kuwa ndio sababu iliyopelekea mwimbaji huyo kushuti video ya Can’t Remember to Forget You na Rihanna ambaye alimshika na mwisho wa siku video hiyo kukosolewa sana kwa madai ya kuhamasisha vitendo vya usagaji.
Alhamisi, Shakira ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuweka sawa kauli yake baada ya kusoma kilichoandikwa na vyombo vya habari.
“Nilikuwa nafanya ucheshi/utani na sasa naona baadhi ya vyombo vya habari vimechukulia kweli! Ukweli ni kwamba tumekuwa na uhusiano mzuri wenye kuaminiana, na wivu haujawahi kuwa issue kwa pande zote.” Ameandika Shakira.
“Nitakuwa makini pindi nitakapokuwa nataka kutumia ucheshi, kama ilivyo wazi inaweza kutafsiriwa tofauti kirahisi.” Ameongeza kwenye post hiyo ya Facebook.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!