Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SOKA KAMWE HALITABIRIKI...PATA HUYU MKUSANYIKO WA MECHI ZA JUZI KUAMKIA JANA.

SOKA KAMWE HALITABIRIKI...PATA HUYU MKUSANYIKO WA MECHI ZA JUZI KUAMKIA JANA.

Written By Unknown on Friday, 18 April 2014 | Friday, April 18, 2014


Uliona kilichotokea katika viwanja vya kandanda barani Ulaya, usiku wa kuamkia jana?.Real Madrid bila, mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo ilitwaa taji la kwanza msimu huu baada ya kuichapa, FC Barcelona magoli 2-1 katika uwanja wa Nou Mestalla, jijini Valencia.
AS Monaco ilichapwa magoli 3-1 ugenini na timu ya Guingamp na kuondoshwa katika michuano ya Coppa de France. Kikosi cha kocha, Claudio Ranieri kilijaribu kufanikisha safari yao ya kwanza kutwaa ubingwa baada ya mshambulizi, Dimitar Berbatov kusawazisha bao la mapema la wenyeji. Ikiwa imepoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Legue 1, Monaco walifungwa katika nusu fainali usiku wa jana licha ya kutumia zaidi ya pauni 100 millioni wakati wa majira yaliyopita ya usajili. Guingamp imefuzu fainali kwa mara ya tatu tangu kuanzishwa kwake.
Uliona kilichowakuta, Everton pale, Gudson Park mbele ya C.Palace?. Najua uliona, walikuwa nyuma ya magoli 3-0, wakajitahidi kufufuka na walipofika katika ubora wao wa Wakajitahidi kupunguza magoli lakini
hayakutosha, wakaishia kufunga magoli mawili katika mchezo ambao walistahili kupoteza katika uwanja wa nyumbani, japokuwa haitarajiwa kabla ya kuanza kwa mchezo huo. Palace inapigana kutoshuka daraja na wanakumbukwa kwa kuzima jaribio la Chelsea kutwaa taji wiki mbili zilizopita. Sasa wameizuia, Everton iliyo katika kiwango cha juu kutinga nafasi ya nne.

Michezo minne ikiwa imesalia, Everton wapo nyuma ya Arsenal kwa pointi mbili na watacheza na timu za Manchester United na Manchester City hivyo kufungwa na Palace ni pigo kubwa kwa kikosi cha Roberto Martinez.
Samir Nasri alifunga goli la kusawazisha katika dakika ya 88 na kuisaidia timu yake ya City kupata pointi walau moja baada ya mchezaji…kufunga mara mbili kwa upande wa timu ya Sunderland katika
uwanja wa Etihad. City ambayo ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji msimu huu, iliangusha pointi nyingine mbili baada ya kuchapwa na Liverpool, wikendi iliyopita. Ikiwa katika uwanja wa nyumbani ilitawaliwa kwa muda mwingi na vijana wa kocha, Gustavo Poyet ambao wapo katina nafasi ya mwisho katika msimamo. Unaweza kutoamini,
ila soka linapigwa kweli barani Ulaya.


Wakati mwingine unajiuliza timu kama Juventus inapangaje matokeo wakati soka uwanjani halioneshi dalili ya uuzwaji wa mechi. Hakuna kupanga matokeo kule. Real iliichapa Barca iliyokuwa ikihitaji kutwaa
kikombe chochote msimu huu baada ya mambo kuwa hovyo katika ligi ya Ulaya na kwenda mrama katika La Liga. Real wanasaka mataji matatu chini ya Carlo Ancelotti, Barca inapotea chini ya Tito Martino! Ndiyo maisha ya soka katika nchi za ulaya yanavyokwenda.


Timu yenye, Lionel Messi, Neymar, Xavi, Iniesta, Fabregas, Sergio inachapwa mara tatu mfululizo, huku vipigo viwili katika mashindano ya mtoano!.Ni rahisi tu, unakuwa na wachezaji wanaojituma na wenye maarifa kama Gareth Bale, anakimbia kwa kasi na mpira kwenda pembeni ya uwanja kisha atachanga maarifa anatumia kasi yake hiyo kuvamia lango la Barca na kuwamaliza. Carlo ni mkali sana wa mbinu na amefungwa mara mbili na Barca msimu huu katika La Liga ila amewachapa bila Ronaldo katika fainali na kutwaa kikombe.
City inapotea mwishoni mwa ligi! Everton inapokea kipigo kutoka kwa timu inayopigania kushuka.Soka linapigwa kwelikweli barani Ulaya...
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi