Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SOMA KILE ALICHO KISEMA KOCHA WA CLUB YA LIVERPOOL

SOMA KILE ALICHO KISEMA KOCHA WA CLUB YA LIVERPOOL

Written By Unknown on Friday, 18 April 2014 | Friday, April 18, 2014

Meneja wa Liverpool,Brendan Rodgers amesema kuwa timu yake itajaribu kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza kwa njia sahihi.
Liverpool inaongoza msimamo wa ligi na kwasasa zawadi ipo mikononi mwao menyewe huku wakijua kama watashinda michezo yote minne iliyobaki basi watakuwa mabingwa.
Rodgers anasisitiza kuwa anataka timu yake kupata mafanikio yao kwa njia sahihi na njia bora zaidi za kimichezo zinazowezekana na sio kwa mbinu ambazo haziko sawa ilimradi watwae taji.
Huku akisema,”Tutajaribu kufanya hivyo kwa njia sahihi.Natumia mbinu bora katika kushinda kwa njia bora zaidi tunazoweza za kimichezo.”
Akaongeza kuwa,”Kama unatuangalia sisi,tunaongoza katika msimamo wa ligi na tunaongoza katika timu zenye nidhamu bora katika ligi.”
“Hatuwazunguki waamuzi.Tunataka kushinda lakini hiyo inakuonyesha wewe alama nzuri ya tabia na nidhamu yetu.”
Pia raia huyo wa Ireland akadai kuwa,”Kuna alama nyingi kubwa ya klabu hii.Ni klabu iliyoshinda mataji mengi kipindi cha nyuma lakini yalikuwa ya heshima na daraja kubwa.”
Rodgers akaendelea kwa kusema,”Neno moja ambalo mara zote nakua nalo katika akili yangu wakati najiunga Liverpool ni ‘Daraja’.Hivyo hilo ni muhimu sana kwangu heshima zote hizo zinarudi.”
“Naamini huwezi kuathiri maamuzi ya mwamuzi.Kutakuwa na baadhi ya bahati zitakuwa mbele yako au dhidi yako lakini napenda kufikiri kama timu ya michezo na timu inayojaribu kufanya kazi vizuri,tumepata tunachostahili mwaka huu.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi