Rais wa Shirikisho la
Soka barani Ulaya, Michel Platini amesisitiza kuwa Paris
Saint-Germain-PSG na Manchester City hazitafungiwa kushiriki michuano ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya kama wakikutwa na hati ya kukiuka sheria ya
matumizi ya fedha. Bodi ya UEFA inayosimamia sheria hiyo imekutana
mapema mwezi huu kufanya uchunguzi wa timu zilizokiuka sheria hiyo
ambapo mbali na PSG na City vipo pia vilabu vingine 76. Bodi hiyo
inatarajiwa kutangaza matokeo ya uchunguzi wake mapema mwezi ujao lakini
Platini tayari ameweka wazi kuwa PSG na City hazitaondolewa katka
michuano hiyo. Platini amesema kutakuwa na adhabu kali kwa timu
zilizokiuka sheria hiyo lakini hakuna yoyote itakayoondolewa katika
michuano ya Ulaya.
Home »
michezo ulaya
» SOMA VILE RAIS WA U.E.F.A ALIVYO ZITETEA TIMU ZA P.S GERMAINT NA MANCHESTER CITY
SOMA VILE RAIS WA U.E.F.A ALIVYO ZITETEA TIMU ZA P.S GERMAINT NA MANCHESTER CITY
Written By Unknown on Friday, 25 April 2014 | Friday, April 25, 2014
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!