Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SOMA VILE RAIS WA ZAMBIA ALIVYO WACHANA WAZUNGU KWENYE KIKAO CHA VIONGOZI WA ULAYA NA AFRICA MJINI WA BRUSSELS

SOMA VILE RAIS WA ZAMBIA ALIVYO WACHANA WAZUNGU KWENYE KIKAO CHA VIONGOZI WA ULAYA NA AFRICA MJINI WA BRUSSELS

Written By Unknown on Saturday, 5 April 2014 | Saturday, April 05, 2014

Rais Michael Sata wa Zambia amesema kuwa, nchi za Ulaya ndio chanzo cha migogoro katika nchi za bara la Afrika.
Rais Sata ameyasema hayo katika kikao cha viongozi wa Ulaya na Afrika, mjini Brussels, Ubelgiji na kuongeza kuwa, uzalishaji wa silaha zisizohitajika na kuyapatia silaha makundi ya waasi katika nchi tofauti za Kiafrika, umepelekea kuongezeka wimbi la machafuko katika nchi za bara hilo. Rais wa Zambia ameenda mbali zaidi na kusema kuwa, hivi sasa watoto wengi wanaoingizwa jeshini, licha ya umasikini mkubwa unaowakabili, wanabeba silaha zenye thamani kubwa ambazo zimetengenezwa na nchi za Ulaya. Swali la msingi ni kwamba, watoto hao wanapata wapi fedha za kununulia silaha hizo licha ya umasikini walionao?, amehoji Rais Michael Sata wa Zambia.
Karibu kila siku raia wa kawaida katika nchi mbalimbali barani Afrika wakiwamo wanawake na watoto hupoteza maisha yao na kuwa wakimbizi kutokana na machafuko yanayotokea barani humo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi