Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » TAARIFA KUTOKA DRC ZASEMA KUWA MAKUNDI YA WAASI YA NCHINI HUMO YARIPOTIWA KUWATEKA WATU NYARA

TAARIFA KUTOKA DRC ZASEMA KUWA MAKUNDI YA WAASI YA NCHINI HUMO YARIPOTIWA KUWATEKA WATU NYARA

Written By Unknown on Saturday, 5 April 2014 | Saturday, April 05, 2014

Watu 32 wanaripotiwa kutekwa nyara na makundi ya waasi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Habari zinasema kuwa, watu hao walitekwa nyara kuanzia tarehe 23 hadi 28 mwezi Machi mwaka huu na wanamgambo tofauti katika eneo la Nindja mkoani Kivu Kusini, mashariki mwa nchi hiyo. Taasisi zinazoshughulikia masuala ya kibinadamu nchini Kongo DRC, zimeelezea kusikitishwa na uungaji mkono wa baadhi ya pande kwa makundi hayo ya wanamgambo ambayo yamekuwa yakitekeleza vitendo vya ukatili nchini humo.
Kufuatia kunshindwa na askari wa serikali kwa kushirikiana na askari wa kimataifa nchini humo, kundi la M23 ambalo ndilo lililokuwa na nguvu zaidi ya makundi mengine ya waasi huko mashariki mwa Kongo, liliamua kuweka chini silaha dhidi ya serikali. Hata hivyo na licha ya hatua hiyo ya M23 kuacha mapigano, bado kuna baadhi ya makundi yanaedesha harakati zake za uasi nchini humo. Wakati huo huo, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) nchini Kongo, imetangaza kuwa, zaidi ya watu laki tano mkoani Katanga kusini mashariki mwa nchi hiyo, wamekuwa wakimbizi ndani ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi