Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » LEO KATIKA HISTORIA JE,ULIKUWA UNA YAFAHAMU HAYA?BASI CHUKUWA MUDA WAKO MDOGO KWA KUYASOMA HAPA

LEO KATIKA HISTORIA JE,ULIKUWA UNA YAFAHAMU HAYA?BASI CHUKUWA MUDA WAKO MDOGO KWA KUYASOMA HAPA

Written By Unknown on Saturday, 5 April 2014 | Saturday, April 05, 2014

Siku kama ya leo miaka 58 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 5 Aprili 1956, yalimalizika mashambulizi ya kinyama ya majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina katika eneo la Ukanda wa Gaza. Majeshi ya utawala ghasibu wa Israel, siku ya tarehe 4 Aprili, yalianza kufanya mashambulio makubwa na kuwauwa watu 56 na kuwajeruhi wengine 30 wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee katika kipindi cha siku mbili. Nchi za Magharibi na jamii ya kimataifa hazikutoa radiamali yoyote kuhusiana na jinai hizo za Wazayuni.

     ********************************************************

Miaka 429 iliyopita katika siku kama ya leo, yalifanyika mauaji ya halaiki katika mji wa Haarlem nchini Uholanzi, ambako kilikuwa kitovu cha wapigania uhuru nchini humo. Mauaji hayo yalifanyika kwa amri ya Mfalme wa Uhispania wakati huo aliyejulikana kwa jina la Philip II. Jumla ya watu elfu sita wanaaminika kuwa waliuawa kwenye shambulio hilo. Hatimaye Uholanzi ilijipatia uhuru wake kutoka kwa mkoloni Uhispania 1609. 

     ********************************************************

Katika siku kama ya leo miaka 220 iliyopita, aliuawa Georges Jacques Danton mmoja kati ya vinara wa mapinduzi ya Ufaransa. Danton licha ya kusomea fani ya sheria, alikuwa mhamasishaji mzuri katika kipindi cha mapinduzi ya Ufaransa. Danton alikuwa akiamini kuwa, sanjari na kuzuia machafuko na maafa ya kibinadamu, utawala wa kifalme nchini Ufaransa ulipaswa kutokomezwa. Hatimaye Danton alitiwa mbaroni kwa njama za
Maximilien de Robespierre mmoja kati ya vinara wakubwa wa mapinduzi ya Ufaransa ambaye pia alikuwa mshindani wake na kisha akanyongwa.

     ********************************************************

Na miaka 426 iliyopita katika siku kama ya leo Thomas Hobbes mwanafalsafa mashuhuri wa Kiingereza alizaliwa. Alimaliza masomo yake katika Chuo Kikuu Oxford nchini Uingereza na alifanya utafiti mkubwa kuhusiana na fasihi. Hobbes alikuwa mtu mwenye kujiona na aliyependa jaha na madaraka.  Kitabu muhimu cha Thomas Hobbes ni Leviathan. Mwanafalsafa huyo wa Kiingereza alifariki dunia mwaka 1679.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi