Msemaji wa Waasi wa RENAMO wa nchini Msumbiji, Fernando Mazanga
ametangaza habari ya kutiwa saini makubaliano ya awali kati yao na
serikali ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, waasi wa RENAMO
watajiunga na jeshi na polisi ya nchi hiyo. Pamoja na hayo Mazanga
amesisitiza kuwa, harakati yake haitaweka chini silaha hadi pale
kutakapowekwa saini makubaliano ya mwisho na serikali ya nchi hiyo.
Hii ni katika hali ambayo kuweka chini silaha ndilo sharti kuu la serikali ya Maputo kwa waasi hao. Waasi wa RENAMO walitia saini makubaliano ya amani na serikali ya chama tawala FRELIMO mwezi Oktoba mwaka 1992, hata hivyo waliamua kuvunja makubaliano hayo mwaka jana na kufanya mashambulizi kadhaa dhidi ya wananchi katika maeneo tofauti ya Msumbiji, hususan katika mji mkuu, Maputo. Serikali ya Rais Armando Guebuza wa nchi hiyo inawatuhumu waasi hao kwa kuvunja makubaliano hayo ya amani. Hata hivyo waasi wa RENAMO wanayataja mashambulizi ya jeshi la serikali dhidi ya ngome zao kuwa ndiko kulikovunja makubaliano hayo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!