Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » WAFUNGWA WA UPINZANI WA MISRI WAENDELEA KUTESWAA

WAFUNGWA WA UPINZANI WA MISRI WAENDELEA KUTESWAA

Written By Unknown on Friday, 25 April 2014 | Friday, April 25, 2014

Gazeti la Financial Times la Uingereza limeripoti kuwa maelfu ya wapinzani wa serikali ya Misri wanaoshikiliwa katika jela za siri za nchi hiyo wanasumbuliwa na mateso na ukatili wa aina mbalimbali.
Financial Times limeandika kuwa wafungwa wa kisiasa pia wanateswa na kudhalilishwa katika jela nyingi za Misri ambazo si za siri kama zile za Turra na Burjul Abar. Limesema kuwa jela za siri nchini Misri zimeongezeka sana baada ya kushadidi wimbi la upinzani dhidi ya mapinduzi ya kijeshi yaliyoiondoa madarakani serikali iliyochaguliwa na wananchi ya Muhammad Mursi. Ripoti zinasema kuwa Wizara za Sheria na ya Mambo ya Ndani za Misri zinakataa kujibu matakwa ya familia za watu waliotiwa nguvuni na kufungwa katika jela za siri ambao wanataka kujua hatima ya jamaa zao.
Wakati huo huo maelfu ya raia wa Misri wameendelea kufanya maandamano katika miji mbali ya nchi hiyo wakipinga mapinduzi ya kijeshi na hatua ya kiongozi wa mapinduzi hayo Jenerali Abdulfattah al Sisi ya kujiandikisha kwa ajili ya kugombea kiti cha rais wa nchi hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi