Kocha wa Borussia Dortmund,Jurgen Klopp
anasema kuwa hajapelekewa maombi yeyote na Manchester United ya kutaka
kupewa umeneja na klabu hiyo ya Old Trafford kufuatia kufukuzwa kwa
David Moyes mapema wiki hii.
Moyes alifukuzwa na Man United Jumanne kufuatia mabingwa hao wa
Uingereza kukalia nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi wakiwa pointi 23
nyuma ya vinara Liverpool huku michezo minne ikiwa imebaki.Klopp amekuwa anapewa nafasi kubwa zaidi ya kuchukua nafasi ya Moyes
lakini akiongea na waandishi wa habari wa Dortmund alisema kuwa
hajapokea ofa kutoka kwa Man United hivyo hakukuwa na kitu chochote
kwake cha kufikiria kuhusu jambo hilo.Huku akisisitiza,”Ukweli nafikiria kwamba Manchester United ni klabu kubwa sana lakini pia ni jambo ambalo ni la muda mrefu na kadri mambo yanavyozidi kwenda ndiyo maana wapo hapa ila nina mkataba na Borussia Dortmund.”
Pia akaongeza kuwa itakuwa kitu cha aibu sana kwake kama atakataa ofa hiyo wakati bado haijakamilika hivyo iwapo atapewa ofa ndiyo anapaswa kuzungumzia kwa kina suala hilo.
Klopp ameiongoza Dortmund kupata mataji mawili ya Bundesliga pamoja na kuifikisha fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu uliopita katika kipindi chake cha miaka sita akiwa kama meneja wa klabu hiyo.
Mjerumani huyo mwenye miaka 46 alisisitiza kuwa anabaki mwenye furaha na amani klabuni hapo na kudai kuwa,”Nafikiri Man United ni klabu kubwa sana lakini bado nafuraha sana hapa kwasababu kuna sababu takribani 1000 ambazo zinanifanya nipende kufanya kazi katika klabu hii.
“Kitu pekee ni hali ambayo lazima ikamilike na ni muhimu zaidi kuliko mikataba,ni vyote vizuri ambavyo vinajumuika pamoja na kuwa na hisia kwamba mimi ni kocha sahihi katika hii timu hiyo ni sababu na sipaswi kufikiria kuhusu kitu chochote.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!