Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
(Arab League) wanatarajiwa kukutana siku ya Jumatatu wiki ijayo
kujadili mgogoro wa Syria. Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Ahmad bin
Hali, amesema mkutano huyo utafanyika nchini Saudi Arabia. Kwa mujibu wa
Ahmad bin Hali, Saudi Arabia ndiyo iliyopendekeza kufanyika mkutano
huo. Hii ni katika hali ambayo, Riyadh imekuwa ikiwaunga mkono magaidi
wanaopigana na serikali ya Rais Bashar Asad kwa kuwapa misaada ya fedha
na silaha.
Saudia ilikuwa mstari wa mbele kushinikiza kusimamishwa uanachama wa Syria kwenye jumuiya ya Arab League. Kufuatia mashinikizo hayo, jumuiya hiyo ilisimamisha uanachama wa Damascus mwezi Disemba mwaka 2011. Tangu wakati huo, utawala wa Aal Saud umekuwa ukishinikiza kiti cha Syria kupewa wapinzani wa Rais Asad lakini nchi kadhaa kwenye jumuiya hiyo zimekuwa zikipinga vikali suala hilo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!