miaka 6 iliyopita, katika siku kama ya leo, tetemeko lenye
ukubwa wa 7.9 kwa kipimo cha Rishta, liliukumba mji wa Sichuan ulioko
kusini magharibi mwa China. Katika tetemeko hilo la kutisha watu wapatao
87,000 walifariki dunia na wengine laki tatu na 80,000 kujeruhiwa.
Aidha tukio hilo la kutisha liliwaacha mamilioni ya watu bila makazi.
*****************************************************************
Siku kama ya leo miaka 1403 kulingana na kalenda ya Hijria
alifariki dunia Abbas bin Abdul Muttalib, ami yake Bwana Mtume SAW na
mmoja wa shakhsia wakubwa wa Kikuraishi. Aliondokea kujulikana kwa tabia
njema, mwenendo mwema, busara na maarifa ya hali ya juu. Baadhi ya
wanahistoria wanaamini kwamba, Abbas bin Abdul Muttalib aliukubali
Uislamu kwa siri kabla ya Bwana Mtume kugura Makka na kuelekea Madina na
alikuwa akimpelekea Mtume habari za harakati za washirikna mjini Makka.
Mwaka wa nane Hijria Abbas bin Abdul Muttalib aliungana na Waislamu na
baada ya Fat'h Makka aliteuliwa na Bwana Mtume kuchukua jukumu la kutoa
huduma ya maji kwa watu wanaozuru Nyumba ya Mwenyezi Mungu, al-Kaaba.
*****************************************************************
Na siku kama ya leo miaka 44 iliyopita, Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio nambari 278 na hivyo likawa
limekubaliana na ombi la wananchi wa Bahrain la kutaka kutumwa nchini
humo, mjumbe wa Umoja wa Mataifa. Mjumbe huyo alisalia nchini Bahrain
kwa muda wa wiki mbili na kukutana na viongozi wa kisiasa na kikabila
waliokuwa na ushawishi nchini humo. Natija ya mazungumzo hayo ikawa ni
Bahrain kutangaza uhuru wake.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!