Home »
michezo ulaya
» ASHLEY COLE AAMUWA KUSTAFUU SOKA LA KIMATAIFA BAADA YAKUPIGWA CHINI NA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA NA NAFASI YAKE KUPEWA KIJANA MNDOGO
ASHLEY COLE AAMUWA KUSTAFUU SOKA LA KIMATAIFA BAADA YAKUPIGWA CHINI NA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA NA NAFASI YAKE KUPEWA KIJANA MNDOGO
Ashley Cole ametangaza
kustaafu soka la kimataifa baada ya kuachwa katika kikosi cha timu ya
Taifa ya England kinachoenda kushirki kombe la dunia nchini Brazil
kuanzia juni 12 hadi julai 13 mwaka huu.
|
Luke Shaw ataenda kombe la dunia kwa nafasi ya Ashley Cole |
Kocha
wa England Roy Hodgson amempigia simu beki huyo mwenye miaka 33 na
aliyeichezea timu ya taifa mechi 107 na kumueleza kuwa hatakuwepo katika
kikosi chake na nafasi yake imechukuliwa na beki wa Southampton, Luke
Shaw.
|
Kwisha habari yake: Cole, aliyeichezea mechi 107 England anastaafu soka la kimataifaNdani: |
|
Huduma yake: Cole aliichezea England katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Albania machi 2001. |
Cole
ameandika kwenye mtandao wake wa Twita na kusema: "Nimepigiwa simu na
Roy, tumekubaliana naye kuwa timu ya England itakuwa na vijana. Nadhani
ni muda muafaka wa kustaafu kuchezea timu ya England sasa".
"Tuna
kocha mkubwa na timu nzuri, nawatakia mafanikio mema. Nitawasapoti kama
shabiki wa kweli. Namshukuru kila mtu aliyenipenda na ambaye
hakunipenda, niamini, naumia sana kutolichezea taifa langu".
Hodgson anatarajia kutangaza kikosi cha timu ya Taifa ya England leo majira ya saa 8:00 mchana.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!