MOJA ya sehemu zinazofanya Ligi Kuu
England ionekane ni ngumu ni namna wachezaji wanavyotumia nguvu, asilimia kubwa
ya wanaotokea Hispania au Amerika Kusini wamekuwa wakipata shida kuendana nayo.
Pamoja na wachezaji kuwa fiti, karibu
kila mchezaji wa timu aliyekuwa akijua wanakutana na Stoke City basi alijua
kweli shughuli ipo na lazima ajiandae mara mbili zaidi.
Sayansi inasema hivi, kila mchezaji
anavyozidi kuwa na umbo kubwa, zaidi anategemea nguvu na anayekuwa na umbo
dogo, tegemeo lake ni ujuzi zaidi.
Katika ligi hiyo ambayo imemalizika
jana, Stoke City ni kati ya timu tatu za ligi hiyo zenye wachezaji wenye maumbo
makubwa zaidi, nyingine ni Man City.
Mabeki wa Stoke City walikuwa
wanasifika kwa ubabe lakini timu nyingi ziliwalalamikia kwa kucheza faulo
‘unprofessional’, yaani si za kiuanamichezo, unaweza kuzilinganisha na zile za
mchangani.
Wakati fulani, Bolton ikiwa katika
Ligi Kuu England ilipewa sana sifa hiyo, lakini baadaye ikahamia kwa Stoke City
ambayo imeweka fora msimu huu kwa kucheza faulo nyingi zaidi ya timu nyingine
zote.
Stoke City imeshika nafasi ya pili kwa
faulo za kiuanamichezo, lakini ikaweka rekodi kwa kuwa na faulo nyingi ambazo
si za kiuanamichezo na zikijumlishwa ndiyo inashika namba moja kwa faulo nyingi
zaidi zilizozaa kadi.
Faulo walizopiga ni nyingi zaidi
lakini hapa zinazungumziwa zile zilizozaa kadi, maana yake zilizidi kawaida
hadi zikasababisha waamuzi kushindwa kuwa wavumilivu na kutoa kadi.
Lakini wakati wanatoa kadi, kuna faulo
za kiuanamichezo na zile zinazoonekana si za kiuanamichezo na zote zimezaa kadi
ingawa inategemea ni nyekundu au njano. Angalia takwimu zenyewe (Takwimu hizo
ondoa mechi za jana).
Stoke:
Kwa faulo za kiunamichezo imefanya 51
ambazo ni za pili kwa wingi kwa zile za kiuanamichezo. Lakini Stoke imeweka
rekodi kwa kuwa na kadi 11 zilizotokana na faulo zisizo za kiuanamichezo.
Maana yake Stoke ina faulo 62
zilizozaa kadi katika mechi zake 37, kiwango ambacho ni cha juu baada ya Aston
Villa yenye 64 lakini Stoke City inaenda juu kwa kuwa ina faulo nyingi zaidi ambazo
si za kiuanamichezo na kudhihirisha kweli ni wababe wala si hadithi.
Aston Villa:
Wana faulo 61 zilizozaa kadi lakini
zote zimehesabika ni za kiuanamichezo, lakini wana tatu ambazo si za
kiuanamichezo. Maana yake idadi yote ya kadi zao bila kujali ni nyekundu au
njano inafikia 64.
West Ham:
Wagonga Nyundo hao, nao wamo kwa viatu
na wamepiga faulo 51 lakini zikahesabiwa ni za kiuanamichezo pamoja na kwamba
zilizaa kadi. Halafu ‘wakachapa’ tatu pia ambazo zikapewa cheo cha kutokuwa za
kiuanamichezo, jumla 54.
Manchester City&United:
Katika mechi 37, yaani kabla ya mechi
za jana, timu hizo zenye upinzani mkali katika Jiji la Manchester, zilifunga
sawasawa kwa faulo zilizozaa kadi. Kila moja ilichapa mara 49 kwa faulo za kiuanamichezo
na tatu zisizokuwa za kiuanamichezo. Maana yake zina jumla ya 52, kila upande.
Spurs pia imekuwa na idadi sawa na timu hizo mbili.
Nyingine:
Arsenal wamekuwa na faulo 41 zilizozaa
kadi za kiuanamichezo lakini pia tatu zisizo za kiuanamichezo. Liverpool ikawa
na 38 za kiuanamichezo na tatu zilizopewa cheo kuwa zisizokuwa za
kiuanamichezo.
Chelsea waliokuwa wanaonekana wababe,
ajabu inaonekana takwimu zinawafuta katika hisia hizo maana wamepata jumla ya
kadi 39, kati ya hizo 35 za kiuanamichezo na nne zisizokuwa za kiuanamichezo.
Picha zaidi hizi hapa chini:
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!