Siku kama ya leo miaka 69 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 8 Mei
1945, vilimalizika Vita vya Pili vya Dunia baada ya Wanazi wa Ujerumani
kusalimu amri bila ya masharti. Ujerumani ilianza kushindwa vita hivyo
tokea mwaka 1943. Vita vya Pili vya Dunia vinahesabiwa kuwa vita vikubwa
zaidi kutokea katika historia ya mwanadamu, kwani karibu watu milioni
55 waliuawa katika vita hivyo vilivyosababisha pia hasara kubwa.
****************************************************************
Siku kama ya leo miaka 112 iliyopita mwafaka na tarehe 8 Mei 1902, mji wa Saint-Pierre uliangamia baada ya kulipuka volkano kwenye mlima Pelee kusini mwa Ufaransa. Watu wasiopungua elfu 30 walipoteza maisha yao kwenye maafa hayo yaliyochukua muda wa dakika tatu tu.

Siku kama ya leo miaka 220 iliyopita sawa na tarehe 8 Mei 1794 aliuawa Antoine Laurent - de Lavoisier mtafiti, mvumbuzi na msomi wa Kifaransa na mmoja kati ya waanzilishi wa elimu ya kemia ya kisasa, baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kukatwa kichwa kutokana na amri ya utawala wa Kifalme baada ya mapinduzi ya Ufaransa. Lavoisier aligundua elementi zinazounda hewa katika utafiti wake. Baada ya hapo, mkemia huyo wa Kifaransa aliweza kuvumbua gesi ya oksijeni. Lavoisier anafahamika kama 'Baba wa Kemia ya Kisasa.'

Na tarehe 8 Rajab miaka 402 iliyopita alizaliwa faqihi na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Sheikh Abu Jaafar Muhammad bin Hassan maarufu kwa jina la Sheikh Hurr al Aamili huko Jabar Amili nchini Lebanon. Alitokea kuwa miongoni mwa maulama wakubwa wa kufanya uchunguzi mkubwa. Sheikh Hurr al Amili ameandika vitabu vingi vya fiqhi na hadithi na miongoni mwao ni kile cha Wasaailu Shia ambacho kina nafasi maalumu katika duru za elimu ya fiqhi.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!