Habari kutoka Uturuki zinasema kuwa,
takriban wachimba migodi 201 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 200
hawajulikani waliko kufuatia mlipuko mkubwa uliotokea kwenye mgodi wa
mkaa katika mkoa wa Manisa ulioko magharibi mwa nchi hiyo. Habari zaidi
zinasema kuwa zaidi ya watu 500 walikuwa kwenye mgodi huo wakati mripuko
ulipotokea jioni ya jana. Meya wa jimbo la Manisa, Cengiz Ergun,
amesema idadi ya vifo inatarajiwa kupanda kwani wachimba migodi wengi
bado wamefukiwa kwenye mgodi huo hadi sasa. Baadhi ya mashuhuda wanasema
walisikia mripuko mkubwa na kisha baadaye wakaona moto mkubwa kwenye
mgodi wa mkaa wa Manisa. Hadi tunakwenda hewani takriban watu 50
walikuwa wameokolewa na shughuli za uokoaji bado zinaendelea. Waziri
Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amevunja safari yake ya Albania na
anatarajiwa kuwasili Manisa leo Jumatano.
Ajali mbaya zaidi kwenye migodi ya
Uturuki kuwahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni ni ile ya mwaka
1992 ambapo wachimba migodi 263 walipoteza maisha baada ya kutokea
mripuko kwenye mgodi mkubwa katika eneo la Zonguldak.
Hizi ni picha kadhaa za tukio:
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!