Akiwa
na umri wa miaka 111, Dkt. Alexander Imich (pichani) wa jiji la New
York ametajwa kuwa mtu mwenye umri mkubwa, kutokana na Rekodi za Dunia
za Guiness.
Imich, ambaye amesema kuwa umri mrefu umesababishwa na vinasaba vyake vizuri, mtindo wa maisha ya kawaida na ya afya.Alizaliwa Czestochowa, Poland, Februar 4, 1903.
Yeye na mkewe, Wela walihamia nchini Marekani mwaka 1953, ambapo mke wake alifariki mwaka 1986. Imich amekuwa akiishi peke yake mjini Manhattan tangu afiwe na mkewe.
Kauli mbiu yake, aliyoaiambia Guiness ni kwamba, “daima fanya unachokipenda na kuwa na upendo nacho.”
Rekodi hii mpya ya mtu mzee duniani ilithibitishwa baada ya kufariki kwa aliyekuwa anaishikilia awali, Arturo Licata wa nchini Italia Aprili 24. Alifariki akiwa na umri wa miaka 111 na siku 357.
Kwa upande wa mwanamke Bibi Misao Okawa (pichani) wa Osaka, Japan mwenye umri wa miaka 116, alizaliwa Machi 5, 1898.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!