Miaka 129 iliyopita katika siku kama hii
mwaka 1885 aliaga dunia Victor Hugo mwandishi na malenga mashuhuri wa
Kifaransa akiwa na umri wa miaka 83. Hugo alikuwa muungaji mkono mkuu wa
mabadiliko kwa maslahi ya matabaka ya wanyonge na masikini nchini humo.
Victor Hugo alijitumbukiza kwenye uwanja wa kisiasa akiwa na miaka 25
na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa mbunge. Lakini ulipofika wakati wa
utawala wa Napoleon wa Tatu alijiengua kwenye uwanja wa kisiasa na
kubaidishwa kwa muda wa miaka 20 baada ya kupinga siasa za dikteta
Napoleon wa Tatu.
--------------------------------------------------------------
Siku kama ya leo miaka 102 iliyopita
yaani mwaka 1912 alizaliwa Herbert Charles Brown mwanakemia wa
Uingereza. Brown alizaliwa mwaka 1912 mjini London na familia yake
ikahamia Marekani kabla hata hajatimu miaka miwili. Alijiunga na chuo
kikuu cha Chicago mwaka 1935 na kusomea kozi ya Kemia na kuendelea na
masomo hadi alipofanikiwa kuwa mhazili wa chuo kikuu. Mwaka 1979
alitunukia tunzo ya Nobel katika taaluma ya Kemia kutokana na jitihada
alizofanya katika ugunduzi wa michanganyiko mipya ya Kemia Kaboni au
Organic Chemistry. Herbert Charles Brown alifariki dunia mwaka 2004.
-------------------------------------------------------------
Na Miaka 34 iliyopita siku kama ya leo
sawia na tarehe Mosi Khordad mwaka 1359 Hijria Shamsiya ulianza mzingiro
wa kiuchumi wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Baada ya
ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, Marekani ilipoteza
maslahi yake haramu nchini Iran. Kwa hivyo ili kuwaweka wananchi
Waislamu wa Iran katika mashinikizo na kuulazimu mfumo wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran usalimu amri, Marekani ilianzisha mzingiro dhidi ya
Iran. Kufuatia uamuzi huo wa Marekani, Hayati Hadhrat Imam Khomeini (MA)
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alitangaza kuwa uhai wa kiuchumi wa
mataifa haufungamani na madola makubwa ya kibeberu. Akiwahutubia
wananchi wa Iran, alisema: "Msiogope hata kidogo mzingiro hii wa
kiuchumi kwani wakituwekea mzingiro wa kiuchumi tutaimarisha harakati
zetu na hili litakuwa kwa maslahi yetu."
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!