Home »
siasa afrika
» HII NDIO TAHADHARI AMBAYO IMETOLEWA NA UN KWA CONGO BRAZAVILLE KAMA ITAENDELEA KUWAFUKUZA RAIA JIRANI ZAO WA CONGO KINSHASA
HII NDIO TAHADHARI AMBAYO IMETOLEWA NA UN KWA CONGO BRAZAVILLE KAMA ITAENDELEA KUWAFUKUZA RAIA JIRANI ZAO WA CONGO KINSHASA
Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya kutokea mgogoro wa kibinadamu,
iwapo Jamhuri ya Kongo Brazzaville itaendelea kuwafukuza raia wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo walioko nchini humo. Taarifa iliyotolewa na
Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO imeeleza kuwa, tokea mwezi uliopita zaidi
ya raia laki moja na elfu thelathini wa nchi hiyo wamefukuzwa kutoka
Kongo Brazzaville.
Martin Kobler Mkuu wa MONUSCO na Zainab Hawa Bangura
Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya ubakaji katika
migogoro wameitaka serikali ya Brazzaville kukomesha mara moja vitendo
vya kuwafukuza raia wa Kongo Kinshasa wanaoishi nchini humo.
|
Martin Kobler |
Viongozi
hao wa Umoja wa Mataifa wameeleza kuwa, hatua ya kuwafukuza raia wa
Kongo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kwamba itasababisha pia
kuibuka maafa ya kibinadamu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Umoja wa
Mataifa umesikitishwa na vitendo vya utesaji, udhalilishaji wa kijinsia
na ubakaji waliofanyiwa raia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati
walipofukuzwa kutoka Kongo Brazzaville.
|
Zainab Hawa Bangura |
Inafaa kuashiria hapa kuwa,
Polisi ya Kongo Brazzaville ilitangaza kwamba kufukuzwa raia hao
waliokuwa wakiishi nchini humo bila vibali, kumetokana na kushadidi
vitendo vya uhalifu na jinai katika nchi hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!