Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HUYU NDIE SENATOR KUTOKA MAREKANI ALIYE MSHUKURU RAIS WA SYRIA ASSAD

HUYU NDIE SENATOR KUTOKA MAREKANI ALIYE MSHUKURU RAIS WA SYRIA ASSAD

Written By Unknown on Tuesday, 27 May 2014 | Tuesday, May 27, 2014

Seneta Richard H.Black wa Jimbo la Virginia nchini Marekani amemtumia barua ya pongezi Rais Bashar Assad wa Syria kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na jeshi la nchi hiyo za kupambana na makundi ya kigaidi yanayofungamana na mtandao wa al Qaeda. Seneta Richard Black wa Marekani ameongeza kuwa, magaidi wanaopambana na majeshi ya Syria ni watenda jinai na kusisitiza kwamba majeshi ya Syria yanapaswa kusimama kidete na kuyatokomeza makundi hayo ya kigaidi. Seneta Black ameonyesha kukerwa na vitendo vya magaidi nchini Syria vya kuwaua kwa halaiki wanawake na watoto na kusisitiza kwamba, Rais wa Syria amekuwa mstari wa mbele katika kuheshimu wafuasi wa madhehebu na dini mbalimbali wakiwemo Wakristo. Seneta wa Virginia amesisitiza kwamba magaidi wanaoungwa mkono na serikali za Magharibi ikiwemo Marekani na zile za Kiarabu kama vile Saudi Arabia na Qatar pamoja na Uturuki ni watenda jinai na wanapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria vya kimataifa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi